Watanzania watano wafariki Afrika Kusini

Watanzania 5 wameripotiwa kufariki kwenye ajali ya moto iliyotokea katika Jengo moja huko Johannesburg nchini Afrika kusini.

Idadi hiyo imethibitishwa na Afisa wa Ubalozi Mwandamizi wa Tanzania Nchini humo, Peter Shija baada ya kutembelea eneo la tukio.

Mbali na idadi hiyo ya vifo lakini pia amesema watanzania wengine 3 wako Hospitali baada ya kupata Majeraha.

Imedaiwa kuwa Jengo hilo lililokuwa chini ya Umiliki wa Jiji la Johannesburg, lilitelekezwa na kuanza kutumiwa Watu waliokosa makazi, wengi wao wakiwa Wahamiaji wasio na vibali.

Kwa mujibu wa Afisa Ubalozi huyo, zaidi ya Watanzania 150 walikuwa wakiishi ndani ya Jengo hilo kabla ya kuteketea kwa moto ambao umesababisha vifo vya Watu zaidi ya 74.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *