Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Watanzania wametakiwa kutowanyanyapaa watu wenye matatizo ya afya ya akili na badala yake wawafikishe katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Mirembe, ili waweze kupatiwa matibabu na kuepuka madhara yanayotokana na tatizo hilo, ikiwemo ongezeko la matukio ya mauaji na ukatili wa kijinsia.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya afya ya akili Duniani iliyofanyika Kitaifa Mkoani Manyara, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema ni vyema kuhakikisha wenye maradhi hayo wanafikishwa mapeka katika Hospitali hiyo, huku akielezea namna walivyojipanga katika kuboresha huduma za afya ya akili katika Mikoa na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Yesige Mutajwa ameeleza athari za matatizo ya afya ya akili kwa jamii ikiweo mauwaji,
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga naye ameelezea mikakati ya kutoa huduma za afya ya akili katika Wilaya zote za mkoa huo huku akiwaomba wataam hao kwenda kutoa huduma hiyo kwa waathirika wa majanga ya mafuriiko.

Adhia, Sendiga amewataka Wanamanyara kujitokeza kwenda kupata vipimo pamoja na matibabu ya afya ya akili ,ambapo huduma hizo zinatolewa kwa muda wa siku nne, kwenye viwanja ya Motel papaa mjini Babati Mkoani Manyara.


