Na Saada Almasi -Simiyu
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) imewataka viongozi vijiji na kata mkoani Simiyu ambao wanaishi katika maeneo yaliyokaribu na pori la akiba la Kijereshi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wao ili kuhamasisha utalii wa ndani mkoani humo.
Rai hiyo imetolewa na mhifadhi wa pori hilo la Kijereshi Rogath Wado mara baada ya kuwachukua viongozi hao na kuambatana nao katika pori hilo kwa lengo la kuwaonyesha utajiri wa vivutio vinavyopatikana katika pori hilo ili wawe mabalozi wazuri.
“Kipindi cha nyuma kidogo muitikio wa wageni wenyeji umekuwa wa chini sana hivyo kati ya jitihada ambazo tumezichukua sisi kawa watu wa hifadhi ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwaonyesha hawa viongozi wao ili wawe mabalozi kwa wananchi wao wajue huku kuna nini” – mhifadhi Wado
Kwa upande wake diwani wa kata ya Lutubiga Agnes Dwasi amesema kuwa mtazamo hasi wa wananchi juu ya gharama kubwa za kufika maeneo ya kitalii ndiyo unapelekea watu wengi kutokuwa na utaratibu wa kutembelea vitutio vyao.
“wengi wanaogopa wakidhalni utalii ni gharama kubwa sana lakini ni tofauti hata mtu wenye kipato kidogo anaweza kutalii na akafurahia,kwa hiyo sisi tutakuwa mabalozi katika maeneo yetu” Diwani Agnes.
Sambamba na hilo suala la ujangili bado ni changamoto katika pori hilo hali inayosababisha askari wa pori hilo kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati kutokana na barabara kuwekewa vizingiti.
“kuna wakati unapigiza simu kwanmba Kijiji cha jirani kumevamiwa na mnyama ukiwa safarini kusaidia wananchi njiani unakuta barabara imewekewa mawe,tunajua ni majangili hiivyo niwaombe tuache mara moja huu uvamizi unatukwamisha kama taifa” mhifadhi Wado.
Nae mkuu wa kituo cha polisi Lamadi Emmanuel Shani amesema kuwa ujangili utapungua na kukoma kabisa endapo kila mtu atachukua jukumu la kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili wafikeeneo la akiba na kudhibiti uovu huo
“tutoe taarifa kila wakati unapoona viashiria vya ujangili tusisubiri itokee tunaangamiza vivutio vyetu hivyo kila mmoja anajukumu la kuzilinda tunu hizi piga simu muda wowote” kamanda Shani
Pori la akiba la Kijeshi linapatikana katika wilaya ya Busega Mkoani simiyu eneo la kusini mwa hifadhi ya Taifa ya Serengenti