Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watano wafariki kwenye mafuriko Arusha

Jeshi la Polisi kwa kushirikia na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha limeopoa miili mitano ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 13, 2023.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Salvas Makweli amesema bado utambuzi wa umri na majina wa miili hiyo iliyoopolewa na Jeshi la Polisi unaendelea kufanyika.

Kwa upande wake, Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Arusha, Osward Manjejele amesema mbali na miili hiyo pia watu sita wameokolewa na wakiwa hai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *