WATANO WA FAMILIA MOJA WAPIGWA RADI NA KUFARIKI NA WATANO WENGINE WAJERUHIWA MBEYA……

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amethibisha kutokea kwa Vifo vya Watu Watano wa Familia moja Wakazi wa Kitongoji cha Nkangi kilichopo Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Watu hao watano wa Familia moja ya Masiganya Scania (39) ambaye ni Mfugaji walifariki dunia baada ya kupigwa radi kwenye kambi ya kuchungia ng’ombe wakiwa wamelala. Waliofariki dunia katika tukio hilo ni Balaa Scania (28), Kulwa Luweja (17), Masele Masaganya (16), Hema Tati (10) na Manangu Ngwisu (18).

“Katika tukio hilo Watu wengine watano walijeruhiwa ambao ni Gulu Scania (30), Manyenge Masaganya (13), Seni Solo (13), Paskali Kalezi (16) na Huzuni Kalezi (19).

Chanzo cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni mvua kubwa iliyonyesha usiku iliyoambatana na radi, Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya Isangawana kwa matibabu zaidi na walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kuwa nzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *