Watalii elfu 14 kutoka Poland waitembelea Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Nchi ya Poland ni miongoni wa Nchi 10 ambazo Raia wake hutembelea Tanzania kwa wingi kwa shughuli za Utalii na hivyo ili kuchochea zaidi Utalii na biashara Wataalamu wa Nchi hizi mbili wameelekezwa kuchukua hatua zitakazowezesha kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Poland kuja Tanzania.



Rais Samia amesema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Poland Andrzej Duda Ikulu Dar es salaam leo Feb 09,2024 na kisha kuongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali waliyokubaliana.



Rais Samia amesema “Watalii Elfu 41 walitutembelea kutoka Poland kwa takwimu za mwaka jana, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita Watalii Elfu 6 kutoka Poland walitembelea Nchi yetu sasa ili kuchochea zaidi Utalii na biashara tumewaelekeza Wataalamu wetu kuchukua hatua zitakazowezesha kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Poland kuja Tanzania na tumeweka ombi letu hilo kwa msisitizo mkubwa kwa wenzetu wa Poland”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *