Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watahiniwa 5900 kesho kufanya mtihani wa Darasa la saba Shinyanga

Afisa elimu wa shule za awali na msingi Manispaa Ya Mkoa Wa Shinyanga mwalimu Marry Macca amesema zaidi ya wanafunzi elfu 5 na mia 9 wa shule za msingi 61 zilizosajiliwa katika manispaa ya mkoa wa Shinyanga wanatarajiwa kufanya mtihani ya kuhitimu elimu yao ya msingi kesho sept 13 na 14 mwaka huu.

Macca ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Jambo Fm na kusisitiza uaminifu katika zoezi hilo la ufanyaji wa mtihani wa taifa kwa walimu wa shule zote za manispaa ya mkoa.

Kwa upande wake mwalimu wa taaluma wa shule ya msingi town Hanael Youze na mwalimu Diana Magata wa shule ya msingi Jomu zilizopa kwenye Manispaa ya mkoa wa Shinyanga wamesema wamewaandaa vyema wanafunzi wao kuelekea kwenye mitihani yao ya mwisho na kuwaomba wazazi kuwapa ushirikiano wa kutosha wanafunzi hao pamoja na kuwatengenezea mazingira rafiki katika kipindi hiki cha mtihani.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu yao ya msingi wamesema wamejiandaa fresh na mtihani huo na wanatajia matokeo fresh kwa maisha fresh ya baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *