Watahiniwa 376 kurudia mtihani wa kidato cha nne

Akitangaza matokeo ya kidato cha nne Jijini Dar Es Saaam, katibu mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Ally Mohamed amesema wamezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 376 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2023 kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo, ambapo watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2024 kwa mujibu wa kifungu cha 32(1) cha kanuni za mitihani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *