WASIRA AWATAKA WATANZANIA KUWEKEZA KWENYE KILIMO, UFUGAJI NA MADINI NCHINI

Na Saulo Stephen, Iramba – Singida.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndg. Stephen Masato Wasira, amewataka Watanzania kuwekeza ndani ya nchi kwa kutumia fursa zilizopo katika sekta za kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini, ili kuongeza ajira, kuinua kipato cha wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Wasira ametoa wito huo Agosti 20, 2026, alipokuwa akizungumza na wanachama pamoja na wakereketwa wa CCM kutoka wilaya za Mkalama na Iramba katika mkutano wa ndani uliofanyika mjini Kiomboi, Wilaya ya Iramba.

Amesema Tanzania ina rasilimali za kutosha zinazoweza kuwanufaisha wananchi endapo wataamua kuwekeza katika uzalishaji badala ya kutegemea fursa za nje, akisisitiza umuhimu wa kutumia sekta hizo kama msingi wa maendeleo ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *