Wasio na Ndoa Watenganishwa Wakidaiwa Kuzuia Nchi Kuendelea

Serikali nchini Burundi imeanzisha kampeni ya kukomesha ndoa zisizo rasmi huku operesheni ya hivi karibuni ikisitisha uhusiano wa wapenzi zaidi ya 900 kaskazini mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali ya Rais Evariste Ndayishimiye, kutangaza kusitisha uhusiano usio rasmi kwa kile uongozi wa nchi hiyo ulichosema wapenzi wanaoishi bila kufunga ndoa rasmi wanafanya dhambi na inazuia nchi hiyo kuendelea.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu operesheni ya kuwasaka wapenzi ambao hawajasajili rasmi ndoa zao iliyoanzia katika mkoa wa Ngozi ambapo Gavana Désiré Minani, amesema hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili watu 900 ambao walikuwa wanaishi pamoja bila kuhalalisha ndoa yao, wametenganishwa.

Gavana huyo ameongeza kuwa operesheni hiyo imefanikiwa kwa asilimia 85, na ilikuja baada ya watoto 3,600 kuathiriwa na ndoa zisizo rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *