Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Washukiwa sita wa mauaji ya rapa AKA wakamatwa

Polisi wa KwaZulu-Natal kutoka nchini Afrika Kusini siku ya jana Jumanne Februari 27,2024 wamesema wamewakamata watu sita wanaohusishwa na mauaji ya Kiernan “AKA” Forbes na rafiki yake, Tebello “Tibz” Motsoane, wamekamatwa.

Viongozi wakuu wa polisi, akiwemo Kamishna wa polisi wa KwaZulu-Natal Lt-Gen Nhlanhla Mkhwanazi amesema mshukiwa wa kwanza tayari alifishwa mahakamani na alikamatwa Aprili 2023.

Washukiwa hao wengine wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi (Februari 29,2024).

Rapa AKA aluwawa Februari 10, 2023 baada ya kuondoka kwenye Mgahawa wa Wish kwenye barabara ya Florida huko Durban.

Hata hivyo Polisi wanasema wanamsaka mshukiwa mwingine ambaye yuko mafichoni baada ya kuibuka habari za kukamatwa huko Eswatini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *