CEO wa Davido Music Worldwide (DMW), Davido ameweka wazi kuwa ameendesha lebo yake kwa muda wa miaka minne na hajawahi kuchukua mtonyo wowote kwa msanii.
Davido ambaye kwa sasa anawasanii wapatao watano kwenye lebo yake ya DMW, amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyofanya na Steve Stoute, “Niliendesha lebo yangu kwa miaka minne, na sikuchukua hata senti moja kutoka kwa wasanii wangu na nilikuwa nalipa video, malazi na kuwahudumia kwa sababu tu nilifurahi kuona nao wanafurahi kwenye mafanikio yangu.”
Akaongeza “Kwa sasa sina budi kuwaeleza wasanii wangu kuwa hii ni biashara, na lazima utumie pesa kutengeneza pesa.”