Wasanii wa Sarakasi wanaofanya kazi zao ndani na nje ya nchi, wameaswa kuwasilisha mikataba yao ya kazi wanazopata BASATA kabla ya kuisaini, ili waweze kupatiwa ushauri wa kisheria utakaowasaidia kuelewa vipengele mbalimbali vilivyomo ndani yamakubaliano hayo.
Hayo yametanabaishwa hii leo Januari 20, 2025 na Wakili msomi, Joseph Ndosi kutoka ofisi ya BASATA wakati anatoa somo la mikataba kwa wasanii katika ukumbi wa TAMISEMI kivukoni jijini Dar es Salaam wakati wa programu ya mafunzo ya kuwajegea uwezo wasanii nchini.

Amesema, wasanii wengi wanaobahatika kupatakazi nje ya nchi, wamekuwa wakifikia makubaliano na kusaini mikataba inayowanyonya na kuhatarisha maendeleo ya shughuli zao kutokana na vipengele vingi kuwabana au vingine kutotekelezeka kabisa.
“Ipo mifano mingi ambayo wamekutana nayo na kufanikiwa kusuluhisha na mengine kushindikana, mfano baadhi ya vipengele vigumu ni vile vinavyowataka wasanii wetu kutumia mahakama za nchi itakayotajwa kwenye mkataba katika suala la kutafuta suluhu baina yao na makampuni ya Sanaa,” alisema Wakili Ndosi.

Ameongeza kuwa, BASATA imejikita kuwawezesha wasanii hivyowasiwe na haraka ya kusaini mikataba wanayopewa bali waiwasilishe ili ofisi ya sheria iweze kuifanyia kazi kwa kushirikianana balozi za nchi husika zilizoko hapa nchini kwa lengo la kujiridhisha uhalali wake na kutoa ushauri wa kisheria bila gharama yoyote.