Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wasakwa kwa kosa la kumbaka na kumuua  mama wa watoto wanne.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 40, ambaye ni mama wa Watoto wanne anayejulikana kwa Jina la Matha Zachariah, Mkazi wa Mtaa wa Makutano Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa amekutwa ameuawa huku akiwa amebakwa na mtu au watu ambao bado hawajafamika.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limefanya jitihada za kufika eneo la tukio kwa hatua za kiuchunguzi zaidi, ambapo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Rukwa ACP Chacha Maro amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikiwa kuwabaini walitekeleza mauaji hayo.


Aidha Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP Mashenene Mayila amewataka wananchi hao kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuzuia kujitokeza kwa uhalifu wa aina hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *