Wasafirishwa kujiunga vikundi vya kigaidi

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama Nchini ni shwari licha ya uwepo wa matishio ya kigaidi na itikadi kali ambapo Wanamtandao wa kigaidi wamekuwa wakiwadanganya Vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 35 kisha kuwasafirisha kwenda kujiunga na vikundi vya kigaidi Nchi za DRC, Msumbiji na Somalia.

CDF Mkunda amesema hayo mbele ya Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu leo January 22,2024 wakati wa Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda Jijini Dar es salaam.

Mkunda amesema Dawa za kulevya, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na ongezekeo la Wahamiaji haramu ni miongoni mwa masuala yanayohatarisha hali ya usalama ndani ya Nchi na kuongeza kuwa matishio hayo yanaendelea kudhibitiwa kwa ushirikiano na vyombo vingine vya usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *