Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wasafirishaji Wa Madini Ya Ujenzi Kahama Waandamana hadi Ofisi Za Madini

Na Wilium Bundala.


Wasafirishaji wa madini ya Ujenzi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameandamana hadi ofisi za mkoa za madini mkoani humo kupinga kitendo cha ofisi hiyo kumkamata dereva mwenzao huku wakiiomba serikali kutenga eneo maalumu la kuchota mchanga ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu wafanye kazi kwa saa 24.


Wakizungumza na Jambo Fm madereva hao wamesema kuwa kwasasa wanafanya kazi mwisho saa 12 jioni hali inayopelekea kushindwa kikidhi mahitaji ya wamiliki wa vyombpo hivyo pamoja na familia zao.


Mmoja wa madereva hao bwana Ibrahimu Obedi amesema kuwa hapo awali walikuwa wanafanya kazi saa 24 ila kwasasa wanazuliwa ikifika saa 12 jioni hali ambayo inawafanya washindwe kupata hela ya tajiri na hela ya kukidhi maisha ya familia zao.


Sambamba na hayo madereva hao wamelalamikia kitendo cha kupandishiwa ushuru bila kushirikishwa ikiwa ni Pamoja na kutoridhishwa na sheria na aina ya ukamataji kwani wanafukuzwa na kuzuiwa kwa mbele hali ambayo inaweza kusababisha ajali.


“Swala lingine hawatushirikishi pindi wanapotaka kubadili bei ya ushuru hali ambayo sisi tunaona kama ni kero kwetu,Lakini pia wanatukimbiza barabarani kwa kutumia gari yao,hali inaweza kusababisha ajali barabarani”.Alisema bwana Japhet Bukune.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amegiza viongozi wa usarishaji wa madini ya ujenzi na ofisi ya madini Mkoa wa madini Kahama kutafuta siku maalamu ambayo watakaa kwa Pamoja na kusikiliza kero zote ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.


“Niwaombe kwa sasa mtawanyike mkafanye kazi nataka mnipe muda kwa siku ya leo nikae na watu madini pia nikae na viongozi wenu ili nisikilize hoja za kwenu zingine ambazo mnazo” Alisema mkuu wa wilaya Mboni mhita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *