BAADA YA UPASUAJI: WAREMBO WAIZIMIKIA PUA YA ZICSALOMA, KASISI ARUSHA JIWE GIZANI

Baada ya Mchekeshaji wa Nigeria, Aloma Isaac Junior kutumia zaidi ya milioni 150 kufanya upasuaji nchini Uturuki, baadhi ya Wasichana Nchini mwake wamekuwa na shauku ya kuolewa naye, huku wengine wakipinga kitendo hicho kwa kusema huo ni umasikini wa fikra.

Wasichana hao kupitia Mitandao ya kijamii wamesema Zicsaloma anatakiwa arudi Nigeria, ili waweze kutimiza ndoto zao za kuolewa na Mwanaume mwenye muonekano wa kitofauti, kitendo ambacho Kasisi wa Kikatoliki, Fr. Kelvin Ugwu hajapendezwa nacho.

Fratery Ugwu amesema, “Watu wengi walio na mali ni maskini katika kujistahi, nidhamu na hawajui kutosheka, nashangaa eti watu wanafurahia huo ni umasikini wa fikra.”

Wengi wamesema baada ya kufanya upasuaji comedian huyo amekuwa na mfanano na Mfalme wa POP Duniani, Michael Jackson (RIP), huku mwenyewe akisema, amefurahi ndoto yake kutimia.

Aloma Isaac Junior, alizaliwa Novemba 7, 1991 na anajulikana kwa jina lake la kisanii Zicsaloma, akijitambulisha kwa jamii kama, mtengeneza skit, mtayarishaji wa maudhui, mwigizaji, Mchekeshaji na mwimbaji.

Alifanyiwa upasuaji wa pua yake katika Hospitali ya Istanbul Rhino Plasty iliyopo nchini Uturuki, kitendo ambacho kimezua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii, (tazama kiambata chini).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *