Wapinzani Wakebehi Mpango Wa serikali Nchini Congo DR

Wabunge nchini Kongo Jumatano hii leo Wameidhinisha mpango wa utekelezaji wa serikali ya Waziri Mkuu Judith Suminwa uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu.

Wabunge wamedhinisha kwa uwingi mpango huo wa utekelezaji ambao vipaumbele vyake vimekusanywa katika nguzo sita ambazo ni kujenga uchumi ili kuunda kazi na kulinda uwezo wa ununuzi, kulinda mamlaka ya kitaifa na usalama wa raia pamoja na mali zao, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, kuimarisha uwezo wa Wakongo kushiriki katika ujenzi wa nchi, kusimamia ipasavyo mfumo wa ikolojia ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, upinzani kupitia, naibu katibu mkuu wa chama cha PPRD, Ferdinand Kambere wanaamini kuwa mpango huo ni pangu patupu tu na kiasi cha bilioni 93 zinazotarajiwa kutumika katika utekelezaji wa Mpango huo wanelezea kwamba kimetajwa tu ili kuwadanganya wakongomani.

Kwa Uamuzi huo ni Dhahiri kwamba hivi sasa Kongo DRC inakuwa na serikali rasmi ambayo imetawazwa Jumatatu ya Juni 10,2024 kuanza  kazi ikiwa ni  karibu miezi sita baada ya Rais Felix Tshisekedi  kumteua  Judith Suminwa kuwa Waziri Mkuu wa Taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *