Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wapenzi wauliwa chumbani

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki ambapo mwanamke amechinjwa huku mwanaume ambaye hajafahamika jina akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 katika Mtaa wa Oysterbay, Kata ya Dodoma Makulu kwenye chumba ambacho mwanamke aliyeuawa Samira Mathias alikuwa amepanga.

Balozi wa Mtaa wa Msaghalale, Isaya Mabijili amesema kuwa alipata taarifa ya tukio hilo majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kufuatwa na Mwenye Nyumba kulipotokea tukio hilo.

Mzee Mabijili amesema kuwa alipoingia ndani ya chumba hicho alikuta miili miwili ya mwanamke na mwanaume imelala huku damu zikiwa zimejaa chumba kizima na ndipo alipofanya utaratibu wa kuwapigia simu polisi katika kituo cha Chimwaga

Aidha, Balozi Mabijili amesema alichokigundua yeye ni kuwa hakuna mtu mwengine aliyefanya mauaji hayo ila watu hao wameuana wenyewe kwa kuchinjana na kisu kwani walikuwa wamejifungia kwa ndani na ndipo waliamua kuuvunja mlango

“Hawa wametendeana wenyewe kwa wenyewe sio mtu mwengine mana mlango ulifungwa wameumizana wenyewe walikuwa na siri zao na wamekwenda nazo” amesema Balozi Isaya Mabiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *