Halmashauri za Wilaya ya Tanga, Muheza na Mkinga zimepatiwa Boti za Ulinzi na Usalama Baharini kwa ajili ya kuongeza doria dhidi ya wahalifu na wavuvi haramu, ambao wamekuwa wakitumia fursa ya udhaifu wa kiulinzi kufanya matukio yanayoharibu Mazingira ya Bahari.
Boti hizo zimetolewa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania kwakushirikiana na wadau wa Maendeleo ‘WILD AID’ kwa ‘CMA’ ya Kimtommwage Kata ya Kigombe wilayani Muheza na ‘BAF BLUE ACTION FUND’waliotoa Boti mbili kwa ‘CFMA’ za Mchoma Bura Tawalani na Kizingani zilizopo katika Halmashauri za Tanga na Mkinga.
Akikabidhi jana Januari 27 Boti hizo katika Kata ya Chongoleani, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Matilda Buriani, alisema Boti hizo zinakwenda kuongeza nguvu kazi kwenye Ulinzi na Usalama Baharini.
“Tunawashukuru sana Mwambao Coastal Community Network Tanzania,kwa Msaada wenu,niwahakikishie kuwa Boti hizi zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na matokeo yake mtayaona,ni lazima kila mmoja wetu awe mlinzi wa Rasilimali za Bahari,ili tunusuru hali ya upatikanaji wa Samaki na viumbe wengine kwafaida yetu sisi na vizazi vijavyo,” alisisitiza .
Batilda aliwataka Wakazi wa Vijiji vinavyouzunguka Bahari kuacha tabia ya kujihusisha na uchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Uvuvi haramu,
“Niwaombe Wakazi mnaoishi pembezoni mwa Bahari,kumbukeni maisha yenu kwakiwango kikubwa yanategemea Bahari,hivyo Ulinzi na Usalama Baharini ni jukumu letu sote,tujitahidi kulinda na kutunza Rasilimali za Bahari,” aliongeza Batilda
Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, Hassan Kalombo, alisema Boti hizo imetolewa kwenye Kijiji hicho kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wavuvi.
“Kijijiji hiki ni moja ya vijiji ambavyo vinawavuvi wengi sana katika mkoa wetu na Wakazi wake asilimia kubwa maisha yao yanaendeshwa kwa Uvuvi, kwahiyo sehemu ambayo inawatu wengi hata uhalifu nao unakuwa mwingi,kwahiyo tumeona tusaidie kuongeza nguvu za kiulinzi Majini”Aliongeza Kalombo
Aidha aliwataka Wakazi wa vijiji ambavyo vimezungukwa na Bahari kujiepusha na uhalifu wa majini ili kuongeza wigo wa uzalishaji wa samaki.
“Niwaombe Wakazi wa maeneo yote yenye Bahari,mjiepushe na uhalifu wa majini ili tuongeze uzalishaji wa samaki,hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na chabadae , lakini pia tutunze Mazingira ya Bahari,tukifanya hivyo tutasaidia kuongeza uzalishaji wa samaki kwa haraka zaidi,” alisisitiza Kalombo.
Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, Mkoa wa Tanga, Ahmed Salim alisema Boti hiyo ni muendelezo wa kusaidia Jamii iishio Mwambao wa Bahari na mapambano dhidi ya uhalifu wa majini hususani Uvuvi haramu na uchafuzi wa Mazingira.
“Moja kati ya majukumu yetu kama Shirika,nikusaidia Jamii kwakugusa maisha ya Moja kwa Moja, tumekuwa tukisaidia mitaji, Elimu ya Mazingira na kuwawezesha kupanda miti, kutoa Boti za Ulinzi na Usalama,hivyo Boti hii tunaamini itasaidia kunusuru kizazi chetu na chabadae,hivyo niwaombe muitunze ili tutokomeze wahalifu majini”Aliongeza Ahmed
Naye Jacob Naila, Ofisa Mfawidhi Idara ya Uvuvi kitengo cha Doria Kutoka Wizara ya Uvuvi, qlisema wanatarajia kufanya kazi ya doria usiku na mchana katika maeneo yote ya Bahari,
“Kupitia Boti hii,tunatarajia kufanya doria kwenye maeneo mbalimbali ya Bahari hii, tunaomba mtupatie Boti nyengine ili tuongeze wigo ya doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga,” aliongeza Mbaga.