Waondokana na adha ya wajawazito kujifungulia njiani

Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo imeendelea kutekeleza mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo baada ya kujenga zahanati katika katika kijiji cha Katembe kilichopo kata ya Nyakabango Halimashauri Ya Wilaya Ya Muleba Mkoani Kagera.

Wakizungumza na waandishi wa habari kutoka mkoa wa shinyanga waliofika kijijini hapo wamesema zahanati hiyo imekuwa msaada kwao kwani hapo awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika kijiji jirani hali ilyopelekea kina mama wajawazito kujifungulia njiani.

Akikitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi huo wa zahanati kaimu afisa anayesimamia idara ya ujirani mwema kati ya hifadhi na vjijiji jirani Robert Focus Mushi amesema mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 119 ambazo zimegharamia jengo hilo pamoja na vifaa tiba.

Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo inapatika pembezoni mwa ziwa Victoria na ilianzishwa mwaka 1977 na hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere pia ni miongoni mwa maeneo machache ambayo unaweza kuwapata wanyama adimu aina ya Sitatunga,Pongo, Ndege wa majini na pia eneo hili ni maarufu kwa ufanyaji wa utalii wa uvuvi wa samaki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *