Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Waomba watoke jela, kabla wake zao hawajaolewa

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewasisitiza wafungwa na mahabusu wanaotarajia kumaliza kutumikia adhabu zao Gerezani waongeze juhudi katika kumuomba Mungu ili wakirudi uraiani wakaanze maisha mapya ikiwa pamoja na wapenzi wao wakiwa salama.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilisha Ziara ya Siku mbili Mkoani Simiyu ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ameeleza kuwa katika Gereza la Bariadi wafungwa na mahabusu Wanaume waliomba msamaha wa Rais ulegeze masharti ili watoke haraka wawahi wake zao kabla hawaja wasaliti.

“Wamenieleza kuwa lengo lao kuomba kulegezewa kwa masharti ya msamaha wa Rais ni kwamba watoke haraka wakutane na wake zao na mimi nikawaambia waendelee kumuomba Mungu wake zao wasitoke nje sababu wao wamefungiwa hivyo basi walioko majumbani watulie wawakute wakiwa salama”.

Amesema Sagini. Aidha amesema, wafungwa na mahabusu wamemtuma afikishe Salamu za Pongezi kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni kwa juhudi za kuboresha mazingira ya mahabusu na magereza tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *