Idara ya Udhibiti wa Taka na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, imesema inatambua mchango wa vijana waliojiajiri katika kazi ya uokotaji makopo, mifuko na vyuma chakavu, kwani wanasaidia usafi wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Afisa wa Idara hiyo, Johness Mwebesa wakati akizungumza na Jambo Fm kuhusu mchango wa vijana hao wanaokota makopo katika utunzaji wa mzingira ndani ya manispaa ya Kahama.

Mwebesa amesema, Serikali inatambua mchango wa vijana hao kwani katika manispaa ya Kahama taka zenye asili ya plastiki zimekuwa adimu kutokana na vijana hao kuzitafuta na Kwenda kuuza ili kujipatia kipato
“Vijana hawa wana mchango mkubwa sana katika manispaa yetu, kwasasa mitaa mingi haina taka zenye asili ya plastiki kwani taka hizi zinakusanywa na vijana na Kwenda kuuza kujipatia kipato,hivyo mitaa mingi mitaro ni misafi kwa takataka hizi zimekuwa fursa kwa vijana kujipatia kipato,” amesema.

Sambamba na hayo Mwebesa amewataka vijaa hao kujiunga katika vikundi ili waweze kuwezeshwa Mikopo ya vijana ili kukuza mitaji yao na kuimarisha ofisi zao na kutambulika.
“Wito wangu kwa vijana wajiunge kwenye vikundi ili waweze kukopesheka kwani serikali ina mikopo kwa ajil ya vijana ili waweze kukuza mitaji yao na kuondokana na umasikini,” aliongeza Mwebesa.

Naye mmoja wa vijana wanaojihusisha na uokotaji na uuzaji wa makopo Maziku Magata amesea kuwa ameamua kufanya biashara hiyo kwakuwa inamsaidia kupata kipato pia wanasaidia ktunza mazingira ya mitaa mbalimbali kwani makop na mifuko ikiachwa muda mrefu inasababisha mitalo kuziba.
“Nimeamua kufanya biashara hii kwani inanipatia kipato mimi Pamoja na wenzangu wawili ambao nimewaajiri hapa,lakini pia kazi yetu inasaidia kuweka mitalo safi kwani makopo na mifuko ikiachwa kwa muda mrefu inaziba mitaro matokeo yake mitalo inaziba na kusababisha mafuriko,” amesema Magata.

Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Kahama akiwemo Peter Mahongo,Charles Mayala na Jenipher Samweli wamesema, vijana hao wanafanya kazi nzuri inayosaidia kuweka mazingira safi na kutoa wito kwa vijana hao kuacha kuchukua vitu vizima katika makazi ya watu kama ndoo,Masuria na baadhi ya vyuma ambavyo bado vinatumika.
“Kwakweli kazi wanayofanya hawa vijana ni nzuri sana na inasaidia kuweka mazingira safi,lakini wapo vijana ambao wanaiba vitu vya watu kama ndoo,mabeseni n ahata vyuma ambavyo vinavyotumika kwenye kazi mbalimbali,” alisema mmoja wa wananchi hao.



