WANNE WACHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KAHAMA

Na William Bundala, Kahama – Shinyanga.

Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni Vibaka wameuwa kwa kuchomwa Moto na Wananchi wenye hasira kali katika Mtaa Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa baadhi ya Mashuhuda wa Tukio hilo wamesema kuwa watu hao wamekuwa wakitekeleza matukio ya kihalifu hasa nyakati za usiku kwa kuwavizia watu kisha kuwapora mali zao na hata kuwajeruhi.

“Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia leo,hawa vijana wapo wengi wanafanya uhalifu katika eneo hili na usiku wa jana wamevamia watu maeneo hay ana wengine wamekatwa mapanga ndipo ukapigwa mwano kuanza kuwadhibiti na ndiyo hali unavyoiona,” qmesema Rajabu Hassan Shuhuda wa tukio hilo.

Sambamba na hayo wananchi hao wameongeza kuwa mtaa huo umekuwa na vibaka wengi na wanafanya matukio hayo nyakati za jioni na kuliomba jeshi la polisi kufanya doria nyakati za usiku eneo la  shule ya msingi Mhongolo.

“Huu mtaa umekuwa na vibaka wengi nyakati za usiku,wanakaa pale kwenye miembe shuleni wanawavizia watu na kuwapora mali zao na hata wengine kukatwa mapanga,tuombe Jeshi letu la polisi liweke doria maeneo ya shuleni nyakati za usiku kwani wamekuwa wakifanya matukio mengi hapa mtaani,” wamesema wananchi hao.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda ya Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema jitihada za kuwatambua watu hao zinaendelea huku akiwataka Wananchi kutojichukulia Sheria wanapokamata Wahalifu bali wawafikishe katika Vyombo va Sheria.

“Ni kweli tukio hilo limetokea ni vijana wan ne ambao wamepigwa mawe na kuchomwa moto,polisi wamefika na wamechukua miili hiyo na kuipeleka hospitali kwa ajili ya utambuzi,Lakini nitoe rai kwa wanachi wa wilaya ya Kahama na Mkoa wa shinyanga kwa ujumla kutojichukulia sheria mkononi sababu kila mtu ana haki ya kuishi” Amesema RPC Magomi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *