Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanawake wengine wawili wajitokeza na kudai kufanyiwa unyanyasaji na muigizaji wa filamu Jonathan Majors

Wanawake wengine wawili wajitokeza na kudai kufanyiwa unyanyasaji na muigizaji wa filamu Jonathan Majors, ambaye miezi miwili iliyopita alikutwa na hatia ya unyanyasaji dhidi ya mpenzi wake wa zamani #GraceJabbari,

Kwa mujibu wa mitandao wa Times , wanawake hao ambao ni  Emma Duncan na Maura Hooper wanadaiwa kuwa Jonathan Majors alikuwa akiwanyanyasa kimwili au kihisia wakati wa mahusiano yao kwa kipindi tofauti kwa kila mmoja.

Huu utakuwa ni mkosi mwingine kwa staa huyo baada ya kampuni ni Marvel  kusitisha mkataba na muigizaji huyo baada ya kukutwa na kesi.

Duncan anadai kuwa mara kadhaa kuanzia 2015 hadi 2019, Jonathan alikuwa akimfanyia vurugu kimwili. Anadai katika pambano moja linalodaiwa kuwa mwaka wa 2016, Majors alidaiwa kumkaba na “kurusha mwili wake chumbani” na kutishia “atahakikisha kwamba hawezi kupata watoto.” Jonathan Majors alikanusha tuhuma hizo.

Hooper, ambaye alichumbiana na Jonathan kutoka 2013 hadi 2015 baada ya kukutana huko Yale, alidai Jonathan Majors alikuwa akimdhibiti sana na “hakuruhusiwa kuongea na mtu yeyote kuhusu uhusiano wao.” Wakili wa Jonathan Majors, Priya Chaudhry, alizungumza akisema Mteja wake alikuwa Mdogo na asiye na usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *