Wanawake ni waoga kupima Saratani

Wanawake mkoani shinyanga wametakiwa kuwa na desturi ya kupima saratani ya mlango wa kizazi mara kwa mara ili kuepukana na changamoto ya ugonjwa huo.

Muuguzi kutoka hospitali ya mkoa wa shinyanga kitengo cha upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama Mariarose Bernard Ameyasema hayo katika mahojiao maalumu na Jambo Fm na kuongeza kuwa umbali wa hospitali isiwe kikwazo cha kuzuia kujua maendeleo ya afya zao.

Aidha Mariarose ameeleza kuwa mwitikio wa akina mama kwa sasa bado si wa kuridhisha licha ya kuwepo kwa huduma hiyo na kuwataka watoto walio chini ya miaka 14 kupata chanjo ya ugonjwa huo inayopatikana katika vituo vya afya.

Katika kujikinga na kuepukana na ugonjwa huo Mariarose ameshauri kuachana mambo ambayo yatapelekea kukumbana na ugonjwa huo ikiwemo kuachana na uvutaji wa sigara na ngono zembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *