Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanawake mkoani Iringa waaswa kutoingia na watoto vilabuni

Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Mkoa wa Iringa Mkaguzi wa Polisi (INSP). Elizabeth Swai amewaasa Wanawake kuacha tabia ya kwenda kwenye vilabu vya pombe na watoto wao kwani kwa kufanya hivyo wanaharibu makuzi ya watoto na kutengeleza kizazi kisichokuwa na maadili mema katika jamii.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria katika kilele cha siku ya wanawake duniani iliyofanyika kiwilaya katika shule ya Sekondari Kalenga iliyopo kata ya Ulanda Mkoani Iringa.

Insp Swai amesema kuwa, Wanawake wanachangia kwa kiasi fulani kutoa malezi mabaya kwa watoto yanayopelekea mmonyoko wa maadili kwani kuna baadhi yao wanaingia na watoto hao vilabuni na maeneo mengine ya starehe jambo ambalo ni kinyume na malezi bora ya mtoto.

Aidha, amesisitiza juu ya kuripoti matukio ya ukatili ambapo amesema wahanga wa ukatili wa kijinsia kwa asilimia kubwa ni wanawake pamoja na watoto hivyo amehimiza kuwalinda watoto katika vitendo hivyo.

Pia, amewataka akina baba wanaopitia changamoto ya ukatili wa kijinsia kutoka kwa wenza wao wasisite Kutoa taarifa dawati la jinsia na watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *