WANAWAKE 200 WAUAWA KWA UKATILI WA KIJINSIA

Wanawake wanaokaribia 200 waliuawa nchini Kenya mwaka 2024, kufuatia matukio ya ukatili wa kijinsia, idadi ambayo ni karibu mara mbili ya ile ya mwaka uliopita ya Wanawake 170 ambao waliuawa mwaka 2023, kutoka 95 kwa mwaka 2022.

Hayo yamefichuka baada ya kutolewa kwa Ripoti ya kila mwaka ya kundi lankupinga vitendo vya unyanyasaji wa Wanawake kwa ushirikiano na Kampuni ya data ya Odipo Dev na chombo cha habari cha Africa Uncensored. 

Mtafiti mkuu wa kundi hilo, Patricia Andago amesema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa Wanawake wa Kenya na hakuna dalili za kuashiria kuwa vitendo hivyo vitapungua.

Suala la unyanyasaji wa kijinsia limeenea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo mwaka jana baada ya Polisi kuwatawanya Wanaharakati waliojaribu kuandamana kupinga mauaji ya wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *