BODABODA WANAOWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU WAONYWA

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limetoa tahadhari kwa wapanda Pikipiki wa Mnanila Wilaya ya Kipolisi Manyovu, kutojihusisha na vitendo vya kusafirisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume na sheria.

Tahadhali hiyo imetolewa Marchi 3, 2026 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Joseph Kilunga wakati akitoa elimu ya utii na sheria bila shuruti na namna bora ya kudhibiti uhamiaji haramu.

Amesema, wapanda Pikipiki hao wanawajibu wa kushiriki kuimarisha usalama kwa kutowapokea, kuwahifadhi na kuwasafirisha raia wa kigeni wanaoingia nchini kinyume na sheria.

Aidha, Insp. Kilungu pia amewataka wapanda Pikipiki hao kutoa taarifa pindi wanapowaona raia wa kigeni wanaoingia nchini kinyume cha sheria, ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *