Wanaotajwa kuhisika na kifo wakana

Promota Sam Larry, ambaye anatuhumiwa kuhusika katika kifo cha mwimbaji Mohbad (27), hatimaye amevunja ukimya kwa kudai hausiki na kifo cha msanii huyo aliyefariki Jumanne.

Kifo cha msanii huyo kimegubikwa na utata kwani Sam Larry, na mmiliki wa Marlian Music ambaye awali alimsaini Mohbad, Naira Marley, wanakabiliwa na vuguvugu kubwa mtandaoni kwa kutuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii huyo ikiwemo kuwashawishi mapromota kumnyima fursa, hivyo kufanya maisha yake kuwa magumu zaidi baada ya kuondoka Marlian Record.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *