Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema yeye ni mzima wa afya na haumwi, huku akiwaambia wale wanaomuombea mabaya kuwa wataugua wao na atashiriki mazishi yao.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo hii leo Okt9bq 10, Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Amesema, “kuna watu wananizushia mara nimekufa, wengine wanasema ninaumwa. Mimi ni mzima wa afya, afya yangu ni nzuri, sina ninapougua, wataugua wao na nitashiriki mazishi yao,” amesema Dkt. Kikwete


