“Wanaokufa kwa njaa ni wajinga”

Waziri wa masuala ya kigeni nchini Uganda Henry Oryem Okello amesema kwamba waganda wanaokufa njaa ni wajinga, miezi kadhaa baada ya baadhi ya maeneo kukumbwa na njaa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, umasikini na ukosefu wa usalama miongoni mwa sababu nyengine.

“Hawa ni wajinga kwa sababu kuna chakula cha kutosha Uganda, Ukifanya kazi kwa bidii kuna ardhi yenye rutba Uganda, hali ya hewa ni bora licha ya mabadiliko kiasi, Iwapo utaweka juhudi maradufu kwa kuamka mapema lima shamba lako na kupanda mbegu na kulinda mimea yako kwa kweli utakosaje kupata chakula ”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *