
Gideon Gregory,Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amependekeza watuhumiwa wa ubakaji watoto wenye umri chini ya miaka Kumi wasidhaminiwe kutokana na uwepo wa ongezeko kubwa la vitendo vya ubakaji wa watoto.
RPC Mallya ameyasema hayo leo Mei 15,2024 Jijini Dodoma kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Aidha ameomba uwepo na nyumba maalum za kuwalea watoto wanofanyiwa vitendo hivyo kama ilivyo kwa waathirika wa madawa ya kulevya kutokana na kukabiliwa na matatizo ya Afya ya akili kwa waathirika.
“Wazazi naomba muanze kuwafundisha watoto wenu kufanya kazi za mikono na kuwa na utamaduni wa kuwasikiliza ili kutatua changamoto wanazozipitia huko wanapokuwa kutokana na dunia kwasasa kubadilika,”amesema RPC Theopista.