Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wananchi wilayani Magu wanufaika na mradi wa BOOST

Wananchi wa Kata ya Kisesa Wilayani Magu wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule mpya ya awali na msingi Idugija iliyogharimu zaidi ya Tshs. Milioni 540 kupitia mradi wa BOOST.

Akizungumzana wananchi wa kata hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo ujenzi miundombinu ya shule na kuhakikisha huduma mihimu zote zinapatikana ikiwa ni pamoja na maji na umeme.

Aidha Mtanda amewataka wazazi kuwapa malezi bora watoto wao na kuwasimamia kielimu ili kupata kizazi bora na chenye uzalendo kwa Taifa lao pamoja na kuendelea kulinda amani ya Taifa.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Benifaxad Chiguru amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi1511 ina vyumba 16 vya madarasa, matundu 24 ya choo, jengo la utawala, ofisi 4 za walimu, madawati 210, viti 30 pamoja na meza 30.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewatembelea watoto 18 wenye mahitaji maalumu walio katika Shule ya msingi Wita na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwaongezea vyerehani na kuwaboreshea miundombinu yao ya kimasomo.

Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka huu Mtanda amewahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura katika zoezi litakaloanza mwezi Oktoba katika kata yao ili wawe na haki ya kushiriki katika zoezi la uchaguzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *