Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wananchi waomba kupewa elimu ya matumizi sahihi ya gesi

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mara limesema linaendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa huo kuhusu matumizi sahihi na salama ya ya gesi za kupikia majumbani,ili kuondoa uwezekano wa kutokea majanga ya moto katika jamii.

Hayo yameelezwa na  Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo Mrakibu Augustine Magere, ambapo amesema ni hatari kuunganisha mtungi wa gesi na kuanza kutumia punde baada ya kuusafirisha umbali mrefu kutokana na mtikisiko,badala yake gesi iachwe ipoe kabla ya matumizi.

Jambo Fm imepita katika baadhi ya mitaa ya Manispaa ya Musoma kuzungumza na wakazi wa mji huo ambapo wamesema licha ya faida lukuki za matumizi ya gesi majumbani,wanaomba elimu iendelee kutolewa ili kuepuka hatari zake.

Kwa mujibu wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mara,hakuna tukio lolote la moto la hivi karibuni,lililosababishwa na gesi kulipuka na kwamba matukio yaliyotokea mwezi januari 2024 ni yale yaliyohusu maokozi,nyumba kuanguka na kuua mtoto kufuatia mvua zinazoendelea zinazonyesha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *