Uongozi wa Klabu ya Yanga umemrejesha Kocha Abdihamid Moalin kama kocha msaidizi wa Pedro Goncalves, uamuzi ambao umetolewa katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mara baada ya kikao hicho kilichofanyika baada ya kupokea ripoti kutoka benchi la ufundi la timu hiyo, Yanga SC wamebaini uwepo kwa changamoto mbili ambazo ni kucheza mechi mechi saba ndani ya siku 21 na uwepo wa wachezaji wanane ambao ni majeruhi.


