Na Saulo Stephen – Singida.
Wananchi katika Manispaa ya Singida Mkoani Singida wametakiwa kufanya usafi wa Mazingira kwa hiari katika maeneo yao na kupanda miti ili kutunza muenekano wa Miji yao pamoja na Manispaa ya Singida kwa Ujumla.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Bi. Yagi Kiaratu wakati akiongea na wananchi wa kata za Utemini na mandewa kwenye zoezi la kuafanya usafi wa mazingira sanjari na kupanda miti kwa ajili ya kutunza Mazingira katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Singida.

“Mji wetu wa Singida ni mzuri tunapaswa kutunza taswira na muonekano wa mji huu kwa kufanya usafi bila shuruti ili kuepuka faini zisizo za Lazima,” amesisitiza Bi.Yagi.
Ameongeza kuwa katika kusimamia hilo halimashauri ya manispaa ya Singida imetunga sheria ndogondogo ikiwemo faini ya kuanzia eli 50 hadi laki 3 kwa watakabainika kukiuka taratibu za utunzaji mazingira.

Aidha Bi. Yagi kiaratu amewataka wananchi wa Manispaa hiyo kuendelea kupanda miti ili kuvuta mvua na kuepuka kuepuka ukataji miti hovyo katika mazingira yanayowazunguka.



