Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wananchi Mara watamani kuona jeshi la zimamoto likitekeleza majukumu yake ipasavyo

Wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara,wamesema wanatamani kuona Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatekeleza majukumu yake ipasavyo ili kufuta dhana zilizojengeka katika jamii kuwa jeshi hilo lina kasumba ya kuchelewa kufika sehemu ya tukio kwa ajili ya kufanya maokozi.

Wakizungumza na Jambo Fm,baadhi ya wakazi hao wamelitupia lawama jeshi hilo wakidai hufika kwenye matukio ya ajali za moto bila maji ya kutosha huku wakishauri namba ya dharura itazamwe upya kwa kuwa imekuwa sio rahisi kupiga na kupokelewa na kituo kinachohitajika kwa muda huo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mara,Mrakibu Msaidizi wa ya Zimamoto Augustne Magere amesema jeshi hilo kwa sasa linafanya maboresho makubwa kiutendaji ambapo amesema mitazamo iliyojengwa na jamii juu ya Zimamoto sio sahihi huku akisisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara limewakumbusha wananchi kutokuziba barabara za dharura kwenye makazi yao sambamba na kuwaonya wanaoharibu miundombinu ikiwemo visima maalumu vinavyotumiwa na jeshi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *