Wananchi wa Rufiji wameeleza matumaini yao kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utasaidia kuboresha huduma za kijamii, hususan afya na elimu, kupitia upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Wakizungumza katika eneo la mradi huo unaozinduliwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan, mkazi wa Rufiji, Abdul Chobo, amesema mradi huo ni wa Watanzania kwa kuwa umejengwa kwa fedha za Watanzania, hivyo wananchi wana wajibu wa kuutunza na kuulinda kwa manufaa ya taifa.

Kwa upande wake, Zainabu Mng’ombe amesema umeme wa uhakika utasaidia kuboresha huduma za afya, akieleza kuwa awali kukatika kwa umeme kulikwamisha huduma muhimu hospitalini, ikiwamo X-ray, Ultrasound na upasuaji.


