Na Afarah Suleiman Babati – Manyara.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Babati mjini Simon Mumbee amesema maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu katika jimbo hilo yanaendelea vizuri, na kuwataka wananchi wa jimbo hilo, siku hiyo ya tarehe 29, kufika kwenye vituo vya kupigia kura kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.
Mumbee amesema hayo wakati Akizungumza na waandishi wa habari na kuongrza kuwa jumla ya wananchi 80,910 katika Halmashauri ya mji Babati wanatarajiwa kupiga kura na jumla ya vituo 206 kutumika katika zoezi la upigia kura katika halmashauri hiyo.

Aidha, amesema kwa wananchi ambao wamepoteza kadi za kupigia kura na waliandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wataruhusiwa kupiga kura endapo atafika katika kituo alichopangiwa akiwa na aidha leseni ya udereva,pasi ya kusafiria au kitambulisho cha nida na majina ya kitambulisho yafanane na yaliyomo kwenye daftari hilo.
Hata hivyo Mumbe ametoa wito kwa wananchi kijitokeza kwa wingi kwenye vituo vyo kupigia kura ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi atakae wasemea katika kipindi cha miaka mitano ijayo.



