Wanamgambo Waua watu zaidi ya 20 Nigeria

Takriban wanachama 23 wa kikosi kazi cha pamoja cha raia nchini Nigeria wameuawa katika mashambulizi tofauti yaliyofanywa na wanamgambo pamoja na genge la utekaji nyara lenye silaha kaskazini mwa Nigeria.

 Jimbo la kaskazini Mashariki la Borno limekuwa Kitovu cha Uasi wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa Islamic State West Africa Province (ISWAP) walitumia kifaa cha milipuko (IED) kulipua gari lililobeba wanachama hao.

CJTF iliundwa kwa mwaka 2013 ili kuzilinda jamii kaskazini mashariki na kulisaidia jeshi kupambana na Boko Haram na baadaye kuitokomeza ISWAP na kikosi hicho tangu wakati huo kimepanuka hadi katika majimbo mengine ya kaskazini ambayo yanakabiliana na magenge ya utekaji nyara yenye silaha.

Mwenyekiti wa CJTF katika eneo la Gamboru Ngala karibu na mpaka na Cameroon Bw. Tijjanima Umar amesema timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri wakati gari lilipokanyaga kilipuzi kilichotegwa barabarani IED.

Watu tisa kati yao walikufa hapo hapo, wakati wengine wawili walipata majeraha makubwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi,ingawa wamezuiliwa kwa kiasi kikubwa na vikosi vya usalama vya Nigeria, Boko Haram na ISWAP bado wamekuwa wakifanya mashambulizi yanayosababisha vifo dhidi ya raia na jeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *