Wanajeshi wahukumiwa kifo kwa kukimbia Vita DRC

Mahakama ya kijeshi katika mji wa Goma huko Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo imewahukumu kifo maafisa nane wa jeshi la Congo, FARDC kwa tuhuma za kukimbia vita na kutoheshimu sheria za kijeshi.

Mwendesha mashtaka amesema makamanda hao akiwemo Kanali Shamba aliyekuwa mkuu wa kikosi cha Makomando pamoja na msaidizi wake walishindwa kuwajibika kwenye uwanja wa mapambano karibu na mji wa Sake wilayani Masisi eneo lililo magharibi mwa mji wa Goma ambako M23 wanaendelea kuchukua udhibiti wa vijiji.

Wakili wa makamanda hao Bwito Jean Richard wa jeshi tiifu kwa serikali amesema mahakama imefanya makosa kutoa adhabu ya kifo kwa wanajeshi hao ambao walikuwa wamejitolea kulipigania taifa na amekata rufaa huku akiionya mahakama kuwa makini na maamuzi yake kwani yanaweza kupelekea wanajeshi wengine kutokwenda vitani.

Nao baadhi ya wachambuzi wamesema hatua hii itawazuia wanajeshi kukimbia mapigano kila mara na kuwaacha waasi kuchukua vijiji.

Makamanda hao watatu ambao miongoni mwa kuna kapteni mmoja na maluteni wawili wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo na mahakama ameziomba pande husika kukata rufaa katika kipindi cha siku tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *