WANAJESHI BURKINA FASO WAZIMA JARIBIO LA KUMPINDUA CAPTAIN IBRAHIM TRAORÉ

Taarifa kutoka Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso, imeeleza kuwa imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi, dhidi ya kiongozi wake, Kapteni Ibrahim Traoré.

Waziri wa Usalama, Mahamadou Sana amesema Wanajeshi wa sasa na wastaafu ndio waliokula njama na kutaka kufanikisha mpango huo.

Wanajeshi hao wanadaiwa kuwa walitaka kutekeleza mpamgo huo kwa kushirikiana na makundi ya kigaidi, wakilenga kushambulia Ikulu wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *