Na Saulo Stephen – Singida.
Waandishi wa Habari Mkoani Singida wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama mahala pa kazi hususani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu 2025.
Hayo yamejiri kwenye Mafunzo ya ulinzi na usalama mahala pa kazi kwa Waandishi wa Habari Mkoani humo yaliyofanyika August 9 ,2025 katika Ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (SINGPRESS) na Mwezeshaji Jamaldini Abuu ambaye ni Mwandishi wa Habari aliyejengewa uwezo na Umoja wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na (IMS).

Katika Mafunzo hayo, miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa katika kulinda usalama wa mwandishi wa habari mahala pa kazi ni pamoja na Usalama wa kisaikologia, Kimwili pamoja na usalama wa kimtandao kwa waandishi wa Habari.
Aidha, Muwezashaji huyo amesitiza kuwa endapo ulinzi na usalama mahala pa kazi utakuwa vizuri kwa Waandishi wa Habari itasaidia kupatikana kwa taarifa zilizokamili na zenye usahihi kwa Jamii.


