Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanafunzi wawili Mkoani Simiyu wapoteza maisha baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji

Wanafunzi wawili waliotambulika kwa majina ya Anna Mayunga (14) na Martha Dickson (13) waliokuwa wakisoma darasa la saba katika shule ya Msingi Mahaha kata ya Bunamhala wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji ambalo lilichimbwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kufika shuleni hapo na eneo la tukio, kisha kutoa maelekezo ya uchunguzi kufanyika juu ya tukio hilo.

“hili eneo naambiwa kuna kina kirefu hapa, watoto wanaachwaje waje huku, waje kuoga na kufua wakiwa wenyewe kwenye eneo hili? Lakini walimu pia na ninyi tunapopewa dhamana ya kukaa na watoto hebu tujiridhishe, ni muhimu tuwe tunapitia attendance kuona ni watoto gani, wako wapi na wanafanya nini, ukiangalia umbali tuliotembea kutoka shuleni hadi hapa ni karibu kilomita mbili, sasa watoto wanatokaje kilomita mbili waje huku na walimu hawajui? Naelekeza uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na hili.” Amesema Simalenga.

Charles Yamungu ni mmoja wa walimu wa shule ya msingi Mahaha ambaye ameeleza ni kwa namna gani watoto hao walitoka shuleni na kwenda katika dimbwi hilo.

“watoto kutoka, mwalimu alikuwa anatengeneza mashine ya photo copy, tuna mashine ambayo ni mbovu, watoto wale walitoka nje ya utaratibu wa mwalimu bila kujua, sasa kuja kusikia kwa sababu na sisi hatukuwepo tayari huku tukio limeshatokea, maji yapo pale shuleni na kila kitu kipo pale shuleni na shughuli zote zinafanyika pale, ufuaji, uogaji, kila kitu hakuna mwalimu anayependa watoto waje huku kuchota maji na maji yapo pale shuleni.” Amesema mwalimu Yamungu.

Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza tukio hilo lilivyotokea na kusema kwamba walisikia kelele za watoto wakipiga kelele za kuomba msaada wakiwa katika dimbwi hilo na walipofika walibaini kuwa kuna watoto wawili wamezama na kuanza jitihada za kuwaokoa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *