Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanafunzi watakiwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limewataka wanafunzi kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya kihalifu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na wanajamii ikiwemo wazazi na walezi wao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rai hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Simiyu ACP. Edith Swebe wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mkula iliyopo wilayani Bariadi, na kusema kuwa kumekuwa na baadhi ya wazazi au walezi ambao wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya ukatili na  unyanyasaji watoto wao hivyo ni vyema taarifa zikatolewa ili wachukuliwe hatua.

Katika hatua nyingine kamanda Swebe amewataka walimu kutowapuuza wanafunzi ambao wamekuwa wakiwafuata kuwaomba msaada wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na badala yake wawasaidie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *