WANAFUNZI WA CHUO CHA UFUNDI SABABA WAPEWA VIFAA VYA KISASA

Na Saulo Stephen – Singida 

Wanafunzi wenye Mahitaji maalumu wanosoma katika Chuo cha Ufundi sababa Mkoani Singida wamepatiwa msaada wa vifaa vya kisasa vitakavyowasaidia katika masomo yao chuoni hapo. 

Vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la Sense International kupitia mradi wao wa kuwazesha vijana wenye mahitaji maalumu. 

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Afisa Mradi wa Sense International Emiliana Protas Rutakyamirwa  amesema kuwa vifaa hivyo wamevitoa kupitia kwa wafadhili wao ambao ni Faroe Island na Hodge Foundation ambapo amebainisha kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi hao na chuo kwa ujumla ili wapate mafunzo bora na ustawi.

” Vifaa hivi ni kwa ajili ya wanafunzi kuwawezesha wanafunzi ili kuwawezesha kuongeza ufanisi wao wa kumudu mazingira na wanapokuwa darasani” Emiliana

Miongoni mwa Vifaa walivyovitoa kwa wanafunzi hao ni pamoja na Printer, Projekta, Kompyuta ,Viti na vifaa vya kufundishia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *