Wanafunzi 783 wa Kidato cha Kwanza katika Shule za Sekondari Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera walioenda likizo ya mwezi wa nne, wanafunzi 8 kati ya hao ndio waliorudi shule huku 775 wakiwa hawajulikani walipo.

Wakiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani la hamashauri hiyo lililofanyika agosti 23, mwaka huu, baadhi ya madiwani wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuweza kuwanusuru watoto hao huku wengi wao wakihusisha utoro huo na wanafunzi kutembea umbali mrefu kutoka wanapoishi kwenda shule.
Wamesema kuwa ili kuweza kukomesha utoro huo ipo haja ya kuanza ujenzi wa hosteli za wananfunzi sambamba na kutoa huduma ya chakula kwenye shule zote.
Akifunga hoja hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyanza Mhe. Leo Lushau ameagiza wanafunzi hao kusakwa popote walipo na kurejeshwa shuleni sambamba na kuagiza kuanza ujenzi wa hosteli kwa kila kata.
Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP. Advera Bulimba ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo ambaye pia alipata nafasi ya kuhudhuria baraza hilo amewaagiza watendaji wa kata kuhakikisha wananfunzi watoro kurudi shule.
Wanafunzi hao ambao hadi sasa hawajaripoti shule wavulana ni 385 na wasichana ni 390 huku shule yenye idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajaripoti ni shule ya sekondari nemba wanafunzi 97.