Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanafunzi 45,693 Kufanya Mtihani wa Darasa La saba Shinyanga

Na Eunice Kanumba,Shinyanga

Wakati wanafunzi wa darasa la saba nchini wakitarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi Septemba 10 na 11 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh. Anamringi Macha awetaka wazazi walimu na wanafunzi kutojihusisha wala kujiingiza katika udanganyifu wa mitihani kwani shule yeyote itakayobainika kufanya udanganyifu serikali haitosita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuifungia shule husika.

RC Macha ameyasema hayo Septemba 10 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mitihani hiyo ambapo amesema kwa mkoa wa Shinyanga maandalizi yamekamilika kwa ufasaha huku akianisha kuwa jumala ya walimu 3339 watasimamia mitihani hiyo.

Aidha Jambo Media imezungumza na baadhi ya wazazi wa watoto wanaotarajiwa kufanya mitihani hiyo ambao wamehaidi kutokujihusiha na udanganyifu wowote ili kutengeneza mazingira ya ufaulu na kuwataka wasimamazi wa mitihani kutotoa fursa za udanganyifu na kuishukuru serikali kwa kuwezesha uwepo wa mazingira mazuri ya upatikanaji wa elimu nchini.

Aidha ili kujiridhisha na maandalizi ya kuelekea katika mitihani hiyo, Jambo Media imefika katika shule ya awali na msingi Mwenge ili kujionea uatayari na maandalizi  kwa wanafunzi katika kuelekea   kufanya mtihani huo ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo Hassan Hemed Amesema maandalizi yote yamekwisha kamilika na kwamba wapo katika hatua za mwisho za kuwajenga vijana kisaikolojia  ili wawe na utulivu katika siku mbiliza utekelezaji wa zoezi hilo muhimu kwa elimu ngazi ya msingi nchini.

Nao baadhi ya wanafunzi wanotarajia kufanya mitihani hiyo kutoka katika shule hiyo wamesema kwamba wamejiandaa vyema na mitihani hiyo huku wakiahidi ufaulu ambapo pia wamewapongeza walimu wao kwa kuwandaa vizuri ili kukabiliana na mitihani hiyo.

Jumla ya shule za msingi 654 na watahiniwa 45,693 wanatarajiwa kufanya mitihani hiyo katika mkoa wa Shinyanga, ambapo wasichana ni 26,165 na wavulana ni 19,628 huku miongoni mwa shule hizo za serikali  ni 593 na  shule binafsi zikiwa ni 61.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *