WANAFUNZI 41,463 KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SHINYANGA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mtihani wa Taifa wa  kuhitimu Elimu  ya Msingi umeanza hii leo Septemba 10, 2025 ambapo kwa mkoa wa Shinyanga jumla  ya Wanafunzi 41,463 wanatarajiwa kufanya Mtihani huo ambapo utahitimishwa Septemba 11, 2025.

Katibu Tawala Msaidizi, Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Mkoa wa Shinyanga, Mwalimu Samson Hango amesema kati ya Wanafunzi hao Wasichana ni 23,938 na Wavulana ni 17,525 huku Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 54, wakiwamo Wasichana 28 na Wavulana 26, ambapo 52 wana uoni hafifu na wawili hawana uoni kabisa.

Amesema, “Mkoa wa Shinyanga tuna jumla ya wanafunzi 41,463 ambao watafanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kuanzia kesho na kesho kutwa.”

Hango pia ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwarubuni watoto, ili wasifanye vizuri mitihani hiyo kwa malengo binafsi kama kuwaozesha mapema, badala yake wawaunge mkono ili waweze kufaulu na kutimiza ndoto zao.

Vilevile, amesema maandalizi yote yamekamilika ikiwamo kudhibiti tatizo la uvujaji wa mitihani, na kufafanua kuwa wasimamizi wamepewa maelekezo ya kuzingatia maadili, uzalendo na kupewa mbinu za kudhibiti vitendo vya udanganyifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *